Ilibaki kidogo tu klabu ya Mbeya City Fc ipate alama zote tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc lakini uzembe wa wachezaji wa klabu hiyo na kushindwa kuhimili presha ya mchezo kuliwafanya Yanga sc kusawazisha mabao yote matatu na mchezo kumalizika kwa sare ya 3-3.
Mbeya city ilianza kupata mabao ya haraka haraka kipindi cha kwanza kutokana na beki ya Yanga sc kutokua na maelewano ambapo mara nyingi Mamadou Doumbia na Zawadi Mauya walioanza kama mabeki wa kati walikua wanajichanganya mara kwa mara na kusababisha mabao hayo yaliyofungwa na George Sangija 3′ na Richardson Ng’ondya 50′ ambapo dakika mbili baadae alifunga bao la tatu.
Yanga sc ambayo kipindi cha pili ilifanya mabadiliko wakiingia Tuisila Kisinda,Benard Morrison,Dickson Job na Jesus Moloko ambao waliongeza ubora na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 64 ya mchezo kwa penati na kisha dakika nne baadae Salum Abubakari akaongeza bao la pili akipokea pasi ya Khalid Aucho na huku watu wakiwa wameanza kuondoka uwanjani Benard Morrison aliipatia Yanga sc bao la kusawazisha na mpaka mpira unaisha matokeo yalikua 3-3.
Kutokana na matokeo hayo Mbeya City inabidi ishinde mchezo wake wa mwisho ili ijinasue na kushuka daraja kunakoikabili kwani mpaka sasa ina alama 31 katika nafas za hatari ya kushuka daraja.