Connect with us

Makala

Yanga Sc Yaibamiza Coastal Union

Klabu ya Yanga sc imefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho nchini baada ya kuifunga timu ya Coastal Union kwa mabao 3-1 katika mchezo wa uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.

Yanga sc katika mchezo huo iliwaanzisha benchi mastaa Stephan Aziz Ki sambamba na kipa Djigui Diarra huku nafasi zao zikichukuliwa na AbouTwalib Mshery na Pacome Zouzoua aliyecheza kama namba kumi.

Maxi Nzengeli aliaandikia Yanga sc bao la kwanza kwa shuti kali dakika ya kwanza ya mchezo ambapo pia alifunga bao la pili dakika ya 15 ya mchezo huo kabla ya Miraji Abdalah kumtungua Mshery kwa shuti kali dakika ya 18 ya mchezo.

Dakika ya 21 ya mchezo Prince Dube alimpasia pasi Mzize ambaye alifunga bao la tatu kwa Yanga sc baada ya kumchambua kipa wa Coastal Union.

Mpaka mapumziko matokeo yalibaki 3-1 ambapo kipindi cha pili timu zote zilishambuliana lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.

Dakika tisini za mchezo huo zilimalizika kwa Yanga sc kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambapo sasa itavaana na klabu ya Songea United kutafuta nafasi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala