Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Nbc msimu wa 2023/2023 klabu ya Yanga sc imefanikiwa kuanza msimu huu vizuri baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya Kmc katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Chamazi Complex jijini Dar es salaam.
Yanga sc ikianza na mastaa wake wapya Pacome Zouzou,Yao Kwasi walioungana na Aziz Ki,Kennedy Musonda na Jesus Moloko katika eneo la ushambuliaji huku beki ikiongozwa na wazawa Dickson Job,Ibrahim Hamad na Nickson Kibabage na golini akisimama Metacha Mnata.
Iliwachukua dakika 17 kuandika bao la kwanza kutokana na kazi kubwa ya Stephan Aziz Ki ambapo Dickson Job akifunga bao hilo na kipindi cha pili dakika ya 58 Aziz Ki alifunga kwa pasi ya Jesus Moloko baada ya kazi kubwa ya Pacome Zouzou ya kutengeneza nafasi ya Kibabage kupiga krosi kwenye eneo la hatari la Kmc.
Hafidh Konkoni ambaye alichukua nafasi ya Kennedy Musonda alifunga bao gumu ambalo mwamuzi alifanya kazi ya ziada kulitafsiri kuwa goli baada ya kipa Wilbol Maseke kuingia na mpira na kuvuka eneo la mstari wa goli.
Konkoni tena alimsetia mpira mzuri Mudathiri Yahaya ambaye aliuchop kiufundi mpira ambao ulimpita kipa na kuandikia Yanga sc bao la nne dakika ya 76 kisha dakika tano baadae Pacome nae alifunga bao la tano kwa staili hiyo hiyo baada ya kipa wa Kmc kutoka golini bila hesabu.
Yanga sc imefikisha alama tatu ikiwa katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ya Nbc huku ikiwa imecheza mchezo mmoja pekee.