Klabu ya Yanga sc imepata mwaliko wa kuhudhuria sherehe za uhuru wa nchi ya Malawi zitakazofanyika Julai 6, 2023 nchini humo ambapo watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya dhidi ya Big Bullets inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema hivi leo Ally Kamwe ambaye ni mkuu wa Idara ya Habari ya Yanga sc alisema kuwa mwaliko huo maalum kwa timu hiyo umetolewa na Rais wa nchi hiyo Mh.Lazarus Chakwela ili kupendezesha shughuli hizo ambapo pia Rais Dk.Samia Suluhu Hassan atahudhuria.
“Tumepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Serikali ya Malawi kucheza mchezo maalumu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi itakayofanyika Julai 6, 2023. Ni heshima kubwa sana kwa Klabu yetu na kwa Taifa kwa ujumla”
“Siku ya maadhimisho tutacheza na Nyasa Big Bullets ya Malawi na Juai 5 tutakutana na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera”Alisema Ally Kamwe
Pia kwa upande wa maandalizi kwa ajili ya msimu ujao Kamwe alibainisha kuwa kikosi cha timu hiyo kitaingia rasmi kambini Julai 10 Avic Town jijini Dar es salaam ambapo mwalimu mpya wa kikosi hicho anatarajiwa kuwasili muda wowote kuanzia sasa.
“Wachezaji wataanza kuripoti kuanzia Julai 10 kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao, wale tulikuwa nao msimu uliopita na tuliowasajili”
“Wachezaji wakishafika kambini ndo tutawatangazia timu itakwenda wapi kama tutabaki Avic Town au nje ya Tanzania”.
Yanga sc inakabiriwa na upinzani mkali kuanzia msimu ujao baada ya kufanikiwa kuchukua makombe yote nchini mara mbili mfululizo ambapo kwa msimu ujao itakua na kazi ya kuthibitisha ubora wake mbele ya Simba sc,Azam Fc na Singida Fountain Gate Fc.