Connect with us

Makala

Yanga sc Wamwalika Samia kwa Mkapa

Uongozi wa Yanga SC umemualika Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kushuhudia mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya KMC katika kilele cha Mwaka mmoja wa Urais wake siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Mkapa.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara amesema kuwa wamwemwalika mkuu huyo wa nchi kushuhudia mchezo huo ikiwa ni ishara ya kushikamana na Serikali katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani baada ya kufariki kwa Hayati John Magufuri.
“Tumemuomba Rais Samia kama ratiba yake haitambana basi awe mgeni rasmi katika mechi yetu na KMC” alisema Haji Manara
Pia Msemaji huyo wa klabu hiyo aliyahamia akitokea Simba sc Haji Manara amesema kuwa mashabiki wa klabu hiyo wataanza kwa kuchangia damu hospitali ya Muhimbili siku ya Ijumaa march 18 ambapo wanayanga 200 wa kwanza kuwahi kuchangia damu watapata zawadi ya jezi bure.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala