Connect with us

Makala

Yanga sc Vs Mbao Fc Yahamishiwa Ccm Kirumba

Klabu ya Yanga sc imeuhamisha mchezo wake wa kombe la shirikisho nchini la Azam Sports dhidi ya Mbao Fc kutoka uwanja wa Benjamin Mkapa mpaka uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza kufuatia uwanja wa Mkapa kuwa na matumizi mengine.

Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika katika uwanja wa Mkapa siku ya Jumamosi Januari 29 lakini taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini imeonyesha kuhamishwa kwa mchezo huo mpaka jijini Mwanza huku muda wa mchezo ukibadirika kutoka saa moja usiku mpaka saa kumi jioni kutokana na uwanja huo kutokua na taa za kumulikia wakati wa usiku.

Yanga sc inatafuta ubingwa wa kombe hilo la shirikisho ambalo msimu uliopita ililikosa baada ya kufungwa mchezo wa fainali na Simba sc mkoani Kigoma.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala