Connect with us

Makala

Yanga sc Vs Azam Fc sasa Kwa Mkapa

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe kupitia akaunti ya Instagram amethibisha mechi ya Yanga vs Azam itakayopigwa Jumatatu Oktoba 23 itachezwa Uwanja wa Mkapa saa 12:30 badala ya Uwanja wa Azam Complex.

Taarifa za awali zilikua kuwa mchezo huo utachezwa siku ya Jumapili oktoba 22 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam lakini sasa mchezo huo umehamishiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo utapigwa siku ya jumatatu oktoba 23.

Katika mchezo ambao Yanga sc atakua mwenyeji hana budi kushinda ili kutengeneza mazingira ya kuwa bingwa mapema kwani baada ya mchezo huo atakutana na Singida Fountian Gate na kisha Simba sc.

Mpaka sasa Yanga sc ana alama 12 katika nafasi ya tatu ya msimamo huku Azam Fc akiwa katika nafasi ya pili na alama 13 na Simba sc akiwa kileleni mwa msimamo na alama 15.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala