Connect with us

Makala

Yanga sc Kutua Nigeria Kibabe

Klabu ya Yanga sc inatarajiwa kuondoka nchini kuelekea nchini Nigeria siku ya Alhamis usiku kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho  dhidi ya River United utakaofanyika siku ya Jumapili jioni nchini humo.

Yanga sc imefanikiwa kufika katika hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho baada ya kuwa kinara wa kundi D huku Rivers United ikiwa mshindi wa pili katika kundi B na hivyo droo iliyofanywa na shirikisho la soka barani Afrika kuwakutanisha katika hatua ya robo fainali.

Yanga sc inapaswa kujipanga zaidi katika mchezo huo ikizingatiwa kwamba Rivers United imekua ni timu kuifunga haswa ikiwa nyumbani ambapo katika hatua ya makundi ilipata ushindi nyumbani dhidi ya timu ngumu ya Wydan Casablanca huku ikiwa katika nafasi ya pili ya kundi B katika ligi kuu ya nchini Nigeria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala