Connect with us

Makala

Yanga sc Kupinga Uviko19,Ebola

Klabu ya Yanga sc imeingia makubaliano na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la kuhudumia Watoto (Unicef) unaolenga kuongeza uelewa kwa Umma kuhusu Chanjo ya UVIKO-19 na kutoa elimu kuhusu virusi vya Ebola.

Mkataba huo umesainiwa mapema hivi leo mbele ya waandishi wa habari ambapo kwa upande wa Yanga sc uliwakilishwa na Rais wa klabu hiyo Eng.Hersi Said aliyeambatana na Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine ambaye alisema “leo ni siku ya Kihistoria kwa Klabu yetu kuingia mkataba mkubwa na shirika kubwa duniani”.

“Mnamo Septemba 20, 2022 serikali ya Uganda ilitangaza mlipuko wa virusi vya Ebola katika eneo la magharibi mwa nchi.
Ni heshima kubwa kuingia mkataba na UMOJA WA MATAIFA. Ni kwa mara ya kwanza katika historia kwa Vilabu vya hapa Afrika Mashariki. Ushirikiano na UNICEF umejengwa katika falsafa ya Klabu yetu ya kusaidia jamii,Tunajulikana kama timu ya Wananchi. Falsafa yetu ni kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili Wananchi,” Rais wa Young Africans SC Hersi Ally Said

“Suala la Uviko-19, UNICEF katika nchi zaidi ya 190 wamekuwa wakiongoza zile juhudi za kuhakikisha watu wanalindwa na chanjo kuwafikia kwa wakati.
Young Africans inajihusisha zaidi na Jamii yetu kuliko timu nyingine yoyote na UNICEF haibagui mshabiki wa timu yoyote ile na hata Young Africans wanapotembelea”.

“Jamii zetu huwa hawabagui mshabiki wa timu zingine, maana hili siyo swala la Ushabiki ni swala la Kijamii na Kitaifa kwa ujumla na kazi ya kuelemisha Jamii yetu tunayoenda kushirikiana na UNICEF tutahakikisha Wapenzi wa mpira na Wananchi wote namna gani wanaweza kujikinga na maradhi haya”.Alisema Kelvin Twisa Mkurugenzi wa Jackson Group ambayo ndio inajihusimamia masuala ya kibiashara na masoko ya klabu ya Yanga sc.

Yanga sc imekua ni mfano wa kuigwa katika kujitoa kwa jamii ambapo imekua na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima na wasiojiweza kupitia ushirikiano wao na Gsm Foundations.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala