Connect with us

Makala

Yanga sc Kileleni Mwa Npl

Klabu ya Yanga sc imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi ku nchini baada ya kuichapa Coastal Union kwa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha Nasreddine Nabi alianza na safu kali ya ushambuliaji akiwaanzi Fiston Mayele sambamba na Stephane Aziz Ki wakisaidiwa na Farid Musa na Jesus Moloko ambapo dakika ya 28 ya mchezo Mayele alifunga bao lake la 12 la katika ligi kuu na la kwanza kwa Yanga sc katika mchezo huo baada ya kuunganisha mpira uliopanguliwa na Kipa wa Coastal Union Mahamoud Mroivili.

Mapema Kipindi cha pili Mayele alifunga goli la pili kwa Yanga sc baada ya kumalizia kazi nzuri ya Aziz Ki dakika ya 47 kisha Feisal Salum alifunga dakika ya 66 akimalizia tena kazi ya Aziz Ki aliyekua mwiba katika mchezo huo.

Baada ya dakika tisini kukamilika Yanga sc imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo ikiwa na alama 44 huku ikiwasubiri Azam Fc katika mchezo mkali wa ligi kuu utakaofanyika Disemba 25 siku ya Jumapili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala