Connect with us

Makala

Yanga “Out” Mapinduzi Cup

Timu ya soka ya Yanga sc imetolewa kwenye michuano ya kombe la mapinduzi baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati na Mtibwa Sugar baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Mtibwa walipata penati 4 huku yanga wakifunga 2 huku Kelvin Yondani na Abdulaaziz Makame wakikosa kwa upande wa Yanga na Abdulhalim Humoud akikosa kwa upande wa Mtibwa Sugar.

Waliofunga kwa upande wa Yanga ni Paulo Godfrey,Balama Mapinduzi huku Jafary Kibaya,Kibwana Shomari na Dickon Job wakipata mikwaju yao.

Mtibwa walisawazisha goli la dakika ya 37 la Deus Kaseke kupitia kwa Kibwana Shomary dakika ya 90+3 na kuelekea Hatua ya matuta ambapo baada ya kuibuka na ushindi watasubiri mshindi kati ya Simba sc dhidi ya Azam fc ili kucheza fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala