Connect with us

Makala

Yametimia,Nabi Aondoka Yanga sc

Hatimaye klabu ya Yanga sc imethibitisha rasmi taarifa za kuachana na kocha Nasredine Mohamed Nabi ambaye amedumu klabuni hapo kwa misimu miwili na kidogo baada kujiunga na klabu hiyo ikiwa inamalizia msimu wa 2020/2021.

Nabi alijiunga na Yanga sc akitokea klabu ya Al-Merrick Fc baada ya kutimuliwa kutokana na kutofanya vizuri na hatimaye kujiunga na Yanga sc aliyoikuta ikiwa katika ujenzi wa kikosi na kufanikiwa kujenga timu imara yenye mastaa walioipa mafanikio ya kutwaa mataji yote ya ndani kwa miaka miwili mfululizo.

Nabi anaondoka Yanga sc baada ya kushindwana katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya ambapo sasa inatajwa kuwa kocha huyo anaelekea nchini Afrika ya kusini kujiunga na timu ya Kaizer Chief kama kocha mkuu.

Katika ajira yake hiyo mpya kocha Nabi anatajwa kuwa atalipwa kiasi cha takribani milioni mia za kitanzania kwa mwezi kama mshahara wake huku pia akiweka sharti la kwenda na wasaidizi wake.

Inasemekana pia kocha huyo ana mpango wa kumchukua mshambuliaji Fiston Mayele kujiunga na klabu hiyo ikiwa ni pendekezo lake la usajili ili kutengeneza safu imara ya kushindana katika ligi hiyo maarufu barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala