Connect with us

Makala

Willian Anukia Anfield

Kiungo anayekipiga ndani ya klabu ya Chelsea iliyo chini ya Frank Lampard,Willian Borges da Silva, inaelezwa kuwa yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Liverpool baada ya kuwa na mvutano kati yake na mabosi wake ambao wanataka kumpa dili la mwaka mmoja huku yeye akihitaji kupewa kandarasi ya miaka miwili.

Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp tayari imeanza hesabu za kuinasa saini yake ili kandarasi yake itakapomeguka ndani ya Chelsea aibukie Anfield.

Borges da Silva mwenye umri wa miaka 31 amejiunga na Chelsea mwaka 2013 na mkataba wake unakaribia kumeguka June,30 mwaka huu pia amecheza mechi 28 kwenye msimamo wa ligi kuu kabla ya kusimama na amefunga mabao 5 na kutoa asisti 5.

sea

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala