Connect with us

Makala

Watatu Kupunguzwa Simba sc

Ikiwa tayari wapo  kileleni mwa msimamo wa ligi kuu kwa alama sita baada ya kushuka uwanjani mara mbili imebainika kwamba kocha mkuu wa timu hiyo Roberto Oliveira ‘Robertinho’ yupo kwenye mipango ya kufyeka wachezaji watatu kabla dirisha la usajili halijafungwa Agosti 31.

Taarifa za ndani yaklanu hiyo zinasema kuwa wachezaji ambao wameshindwa kulishawishi benchi la ufundi na sasa uongozi unafikiria kuwatoa kwa mkopo ama ikishindikana kuwauza kabla dirisha la usajili halijafungwa.

Kutokana na hilo mastaa kama Jimyson Mwanuke, kipa Ahmed Feruz na mshambuliaji Mohamed Mussa wapo katika hatihati ya kuwekwa sokoni kwa sasa kutokana na  mapendekezo ya kocha Robertinho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala