Connect with us

Makala

Wamebebwa

Ndizo kelele ambazo zinasikika kwa mashabiki wa soka nchini hususani wale wa Simba sc na Azam Fc wakilalamikia matokeo ya sare ya 2-2 baina ya Yanga sc na Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu uliomalizika usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Azam Fc ilikua ya kwanza kuandika bao katika mchezo huo likifungwa na beki Daniel Amoah dakika ya 25 ambalo lilidumu mpaka wakati wa mapumziko ambapo Yanga sc walisawazisha bao hilo dakika ya dakika ya 59 kupitia kwa Feisal Salum aliyepiga shuti kali baada ya beki wa Azam Fc  kuokoa krosi ya Morrison na kumkuta mfungaji.

Bao hilo halikudumu sana kwani dakika sita baadae Azam ilipata bao la pili kupitia kwa Malick Ndoye baada ya uzembe wa mabeki wa Yanga sc kuokoa mpira wa kona lakini walifanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Feisal kwa shuti ambao golikipa Ally Ahmada alizembea kuliokoa na kuzaa bao.

Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa Yanga sc na Azam fc ziligawana alama ambapo Yanga sc imefikisha alama saba kileleni mwa msimamo na Azam Fc wakifikisha alama tano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala