Ndio taarifa inayosubiriwa na wadau wengi wa soka hapa nchini Tanzania baada ya habari za uhakika kuvuja kuwa staa wa klabu hiyo Fiston Mayele amepata ofa kubwa kutoka klabu ya Pyramid Fc ya nchini Misri.
Ofa hiyo ambayo imebadili kila kitu katika mipango ya klabu ya Yanga sc ya kumbakisha staa huyo inakadiliwa kufikia kiasi cha Dola za kimarekani milioni 1.2 ambazo ni takribani shilingi bilioni 2.8 za kitanzania huku pia staa huyo akipokea dau la usajili kiasi cha shilingi milioni 400 pamoja na mshahara wa milioni 80 kwa mwezi.
Mayele tayari amewataarifu mabosi wa Yanga sc kuhusu kutaka kuondoka ili kupata fedha hizo huku pia ikizingatiwa kuwa mchezaji huyo amebaki na mkataba wa mwaka mmoja hivyo ni vigumu kwa klabu hiyo kukataa pesa hizo.
Inatajwa kuwa mabosi wa Yanga sc tayari wamekubali ofa hiyo ya Pyramids Fc na kuzipiga chini ofa za zingine kutoka Uarabuni ambazo zilikua hazifiki kiwango hicho na sasa tayari wameanza kukamilisha baadhi ya masuala madogo madogo ili kumalizana na Pyramids na kutoa taarifa rasmi.
Yanga sc baada ya kupata uhakika wa kuingiza kiasi kikubwa cha hela tayari wameanza mchakato wa kusajili mshambuliaji mbadala wa Mayele huku wakitupa macho yao kwa Makabi Lilepo wa Al Hilal,Sinkara Karamoko wa Asec Mimosa na Andy Boyeli wa Power Dynamos ya nchini Zambia pamoja na Sudi Abdala ambaye ni mchezaji huru.