Connect with us

Makala

Tff Kufikia Muafaka

Kikao cha kamati ya uongozi cha TFF kimeazimia  baada ya siku 30 Serikali itakaporuhusu michezo kuendelea, mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili na Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) zitachezwa bila watazamaji ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo mara baada ya kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na rais wa TFF, Wallace Karia.

Amesema pia kuwa wachezaji wote watafanyiwa vipimo maalum kuchunguzwa endapo wameathirika na virusi vya Corona  kabla ya ligi hizo kurejea.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala