Connect with us

Makala

Taa Zawaponza Maafisa Wizarani

Wizara ya Utamaduni,Sanaa na michezo iliyo chini ya Waziri Balozi Dkt Pindi Chana imeamua kuwasimamisha kazi wafanyakazi takribani saba wanaohudumu katika uwanja wa Benjamini Mkapa kufuatia kuzimika kwa taa za uwanja huo wakati wa mchezo wa kombe la shirikisho baina ya Yanga sc dhidi ya Rivers United siku ya Jumapili.

Miongoni mwa waliosimamishwa kazi ni Kaimu Meneja wa uwanja Salum Mtumbuka,Mhandisi wa masuala ya umeme Manyori Juma Kapesa na Tuswege Nkupala ambaye ni Afisa Tawala wa uwanja huo huku baadhi ya wafanyakazi wa uwanja huo nao wakisimamishwa akiwemo Gordon Nsajigwa,Gabriel Mwasele,Yanuari Imbolu na Dkt.Christina Luambano huku akimteua Bw.Milinde Mahona kuwa kaimu meneja wa uwanja huo.

Kusimamishwa huko kwa wafanyakazi hao kunakuja baada ya tukio hili kujitokeza kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza ilikua ni katika mchezo dhidi ya Taifa Stars na Uganda ambapo taa hizi zilizimika kwa muda wa takribani dakika 15.

Uwanja wa Benjamini Mkapa ni moja ya viwanja vikubwa barani Afrika ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji wanaokadiriwa kufikia elfu sitini kwa wakati mmoja wakiwa wamekaa.

Katika mchezo huo Yanga sc ilifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kutoka suluhu na Rivers United katika mchezo wa pili huku awali Yanga sc ikishinda kwa mabao 2-0 nchini Nigeria.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala