Connect with us

Makala

Sven Akubali Uwezo Wa Miqussone

Kocha mkuu Simba Sc, Sven Vandenbroeck ameweka wazi kuwa kwa sasa anahitaji viungo wakali wenye uwezo kama Luis Miqussone ambao anaamini watampa matokeo ndani ya uwanja.

Miqusssone ambaye ni kiungo wa Simba Kabla ya Ligi kuu bara kusimamishwa ili kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona alianza kuingia kwenye mfumo wa Sven kutokana na kubadili matokeo akiwa ndani ya uwanja licha ya kutumia dakika chache.

Mbelgiji huyo ametoa mapendekezo yake ya aina ya wachezaji anaowataka huku akisisitiza anahitaji viungo wenye uwezo wa kunyumbulika zaidi kama ilivyo kwa Miqussone.

Akiwa ni mchezaji aliyejiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu Januari ,Miqussone alicheza mechi nane na kufunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao lililofungwa na Meddie Kagere kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala