Baada ya kumuuza straika wake Heritier Makambo kwenda Guinea basi Yanga haijalala fasta inashusha straika matata kutoka nchini Nambia anayeitwa Sadney Ulikhob mwenye miaka 27 mzaliwa wa jiji maarufu la windhoek nchini humo.
Straika huyo mwenye urefu wa futi tano na ushee ni mchezaji huru kwa sasa baada ya kumalizana na timu yake ya Psms Medan ya nchini Indonesia aliyojiunga nayo mwaka 2018 huku akiweka rekodi ya kufunga mabao 9 katika mechi 11.
Straika huyo aliyewahi kuja kufanya majaribio katika klabu ya simba ambapo taarifa zinadai alimvutia mbeligiji Patrick Aussems, pia amewahi kuichezea klabu ya Amazulu ya nchini Afrika Kusini mwaka 2013 -2014 akiifungia mabao 9 katika mechi 20 pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Namibia.
Inaripotiwa kwamba mchezaji huyo anakuja kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo ya mwisho na klabu hiyo kisha kusaini kama watafikia muafaka.
Pia yanga iliyopata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika tayari imeshaini wachezaji kadhaa huku ikisadikiwa beki kutoka Burundi Mustapha Suleiman tayari ameondoka nchini baada ya kumalizana na wanajangwani hao huku tayari Patrick Sibomana,Issa Bigirimana,Abdulazizi Makame,Lamine Mollo,Farouk Shikallo,Kalengo Mybin wakiwa tayari wameshasaini kukipiga jagwani hapo wakiwa ni mapendekezo ya kocha Mwinyi Zahera.