Connect with us

Football

Stars Yatoboa Afcon 2024

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani kuanzia 13 Januari mpaka 12 Februari nchini Ivory Coast ambapo jumla ya mataifa 24 yatashiriki michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya timu za Taifa barani Afrika.

Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kutoka suluhu na Algeria katika mchezo wa ugenini na kufanikiwa kufikisha alama 8 ambazo hazikuweza kufikiwa na Uganda licha ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Niger.

Kocha Adel Amrouche aliamua kuanza na ukuta wa chuma akiwatumia walinzi watano Ibrahim Hamad,Dickson Job,Bakari Mwamnyeto,Novatus Dismas na Haji Mnoga akilenga kujilinda zaidi huku akiwaachia Algeria wamiliki mpira kadri wawezavyo kiasi cha mchezo kumalizika Stars ikimilika mpira kwa asilimia 19 tu.

Kibu Dennis alifanya kazi kubwa eneo la ushambuliaji akiwanyima uhuru walinzi wa klabu hiyo kwa kuanza kuwakaba kuanzia juu na kuwasababisha kukosa utulivu.

Pamoja na kushambuliwa kila mara safu ulinzi na kiungo ya Stars inastahili pongezi kutokana na kutimiza majukumu kwa asiliamia 100 ambapo safu ya kiungo Sospeter Bajana na Muzamiru Yassin walifanya kazi ipasavyo.

Hii ni mara ya tatu katika historia ya Tanzania kufuzu michuano hiyo ambapo Rais Samia ametoa jumla ya milioni 500 kama zawadi kwa wachezaji na benchi la ufundi la timu ya Taifa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Football