Connect with us

Makala

Stars Yatinga Makundi,Kaseja Ang’ara

Timu ya taifa ya Tanzania(Taifa Stars) imetinga hatua ya makundi ya kufuzu kombe la dunia baada ya kufanikiwa kuitoa Burundi katika hatua ya pili kufuatia kuibuka na ushindi kwenye mchezo uliofanyika leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Stars ilikua ya kwanza kupata goli dakika ya 29 baada ya Mbwana Samatta kutumbukiza mpira wavuni kufuatia kona ya Mohamed Hussein bao ambalo halikudumu kufuatia kusawazishwa na Abdul Razack dakika ya 45 na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 huku matokeo ya jumla kubaki 2-2 kufuatia matokeo ya sare katika mechi ya awali iliyofanyika burundi.

Licha ya mchezo kuongezwa dakika 30 bado matokeo yalisalia hivyo hivyo na kulazimika hatua ya matuta ifuatie na ndipo kipa wa Star Juma Kaseja alipoibuka staa baada ya kupangua penati ya kwanza huku zingine mbili zikipigwa nje ikiwemo ya staa Saido Berahino anayeichezea Zulte Waregem ya Ubeligiji huku kwa upande wa stars Erasto Nyoni,Himid Mao na Gadiel Michael wakikwamisha mikwaju yao nyavuni.

Stars itaungana na timu zingine 39 kuunda makundi 10 yenye timu 4 ambayo watacheza katika mtiririko wa Nyumbani na ugenini na mshindi wa kila kundi atacheza hatua ya mtoano ili kupata timu tano zitakazokwenda qatar mwaka 2022.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala