Connect with us

Makala

Stars Yalala 2-0 kwa Algeria

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) imekubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Algeria katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon mwakani zitakazofanyika nchini Ivory Coast.

Katika mchezo huo wa pili kwa Stars katika kundi baada ya awali kupata sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Niger,iliwalazimu Algeria kusubiri mpaka mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupata bao la uongozi kupitia kwa Amir Selmane aliyefunga kwa kichwa kutokana na uzembe wa mabeki wa Stars kuokoa mpira wa faulo.

Kocha Kim Poulsen Kipindi cha pili aliweza kufanya mabadiliko kwa  kuwaingiza Kibu Dennis, George Mpole, Kelvin John na Salum Abubakar huku waliotoka ikiwa ni Feisal Salum,Simon Msuva,Nickosn Kibabage na Novatus Dismas ambao walibadili mchezp lakini hawakuwa na madhara kwa wageni kwani mashambulizi mengi yalidhibitiwa kabla ya kufika kwa kipa.

Wakati Stars ikisaka bao la kusawazisha Algeria walipata mpira na kufanya shambulio la kushtukiza na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Mohamed El Amine dakika ya 89′ na kufanya mchezo kumalizika kwa Stars kupoteza alama tatu muhimu.

Kutokana na matokeo hayo sasa Algeria anaongoza kundi F akiwa na alama 6 huku Niger akiwa na alama 2 na Tanzania na Uganda zikiwa na alama 1 kila mmoja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala