Connect with us

Makala

Stars Vs Uganda Bureee

Shirikisho la soka nchini Tanzania (Tff) limetangaza kutokua na kiingilio katika kuushuhudia mchezo baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania itakayocheza mchezo dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) utakaofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mchezo unatarajiwa kuanza majira ya saa mbili usiku ambapo milango itakua wazi kuanzia saa sita mchana tayari kwa mashabiki kuweza kuingia ambapo tiketi zote za mchezo huo zimeshalipiwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini pamoja na serikali.

Rais Samia Suluhu Hassan yeye amelipia jumla ya tiketi elfu saba maalumu kwa mashabiki huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa naye akilipia tiketi elfu mbili ambapo pia wadau wengine akiwemo mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amelipia tiketi mia mbili huku Viongozi wa klabu ya Simba sc Murtaza Mangungu akilipia tiketi 600 na Salim Mhene akilipia tiketi 500.

Wadau hao na wengine mbalimbali akiwemo Rais wa Yanga sc Hersi Said alielipia tiketi elfu moja mia tano pamoja na wengine kama benki ya Crdb iliyolipia tiketi elfu moja wamefanya mchezo huo uwe bure kwa watanzania wote ili kuongeza hamasa ambapo Stars inahitaji kushinda mchezo huo na ikitoa sare mchezo dhidi ya Niger itakua imefuzu fainali za mataifa ya Afrika zitakazofanyika nchini Ivory Coast mwakani.

Mpaka sasa katika msimamo wa kundi F Algeria yupo kileleni na alama 12 huku Tanzania ikiwa nafasi ya pili na alama nne na Uganda wapo nafasi ya tatu na alama 2 huku Niger wakiwa mkiani mwa kundi na alama moja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala