Connect with us

Makala

Stars U17 Wapigwa Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 Serengeti Girls ambayo inashiriki michuano ya kombe la dunia la wanawake linalofanyika nchini India imepoteza mchezo wake wa kwanza baada ya kukubali kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Japan katika mchezo uliokua na ufundi mwingi na wa kusisimua.

Tanzania iliruhusu kipigo hicho cha Magoli 4 – 0 kutokana na kupata kadi nyekundu mapema katika kipindi cha kwanza ambapo mpaka mapumziko ilikua imefungwa 1-0 lakini kipindi cha pili ilikutana na mvua hiyo ya mabao baada ya kulazimika kucheza pungufu kwa muda mrefu.

Akizungumza na timu hiyo mara baada ya mchezo uliochezwa Oktoba 12, 2022 Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul,ameendelea kuwatia hamasa na moyo Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Umri wa miaka 17 Serengeti Girls inayoshiriki Kombe la Dunia nchini India.

“Watoto wetu wanauwezo, wameonesha mpira wa kiwango kikubwa sana, wamekua na ari muda wote wa mchezo, zaidi nampongeza Golikipa Zuhura kwa kuokoa magoli mengi yaliyoelekezwa golini kwetu” amesema Mhe. Gekul.

Serengeti Girls pamoja na kupoteza mchezo huo bado ina nafasi ya kufanya vizuri na kusonga mbele ambapo sasa imebakisha michezo miwili ambapo mchezo unaofata watacheza na Ufaransa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala