Connect with us

Makala

Sisi Tuna Mbrazili,Nyie Mghana

Mashabiki wa Simba Sc walikuwa na kazi moja tu Juzi ya kujitokeza uwanja wa taifa Dar na kuwajibu watani wao Yanga kuwa ‘Nyie mna Mghana sisi tuna Mbrazili mfunga  mabao’

Waliipata jeuri hiyo baada ya kiungo wao Gerson Fraga raia wa Brazil kufunga mabao mawili na kuwapa pointi tatu  Simba mbele ya Coastal Union.

Fraga alifunga bao la kwanza kwa kichwa akiunganisha krosi ya Clatous Chama dakika ya saba kipindi cha kwanza huku bao la pili alimalizia kirahisi na mpira uliopigwa na Hassan Dilunga dakika ya 78 na kuifanya Simba kuibuka kifua mbele.

Simba wanazidi kukaa kileleni wakiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 18 na kushinda mechi 15 huku wakiiacha Yanga pointi 19 ikiwa imecheza mechi 15.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala