Connect with us

Makala

Singida FG Kambi Tunisia

Taarifa za ndani zinasema kuwa mabosi wa klabu ya Singida Fountain Gate wanafikiria kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini Tunisia kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa ambayo wanatarijiwa kushiriki kuanzia msimu mpya unaoanza mwezi julai mwaka huu.

Timu hiyo kutokana na kumaliza ligi kuu katika nafasi ya nne wamefanikiwa kujikatia tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho pamoja na Azam Fc huku Yanga sc na Simba sc wakikata tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Timu hiyo sasa ina misuli ya fedha baada ya kuuzwa kwa Taasisi ya Fountain Gate ambapo imebadili jina kutoka Singida Big Stars kuwa Singida Fountain Gate huku tayari ikifanikiwa kuwasainisha mikataba mipya mastaa wake ambao walikua wanahusishwa na timu za Simba sc na Yanga sc ambao ni Bruno Gomes na Yussuph Kagoma.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala