Connect with us

Makala

Simba,Namungo Kufungua Msimu Mpya

Msimu mpya wa ligi kuu utafunguliwa Agosti 29 wakati Simba Sc ambao ni mabingwa wa ligi kuu wakiwakaribisha Namungo Fc kwenye mchezo wa ngao wa jamii utaochezwa mkoani Arusha,uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mchezo huo ni ishara ya ufunguzi wa msimu wa ligi kwa mwaka 2020/2021 kwani ngao ya jamii huwakutanisha bingwa wa ligi kuu pamoja na bingwa wa ASFC ambapo Simba ndio waliotwaa ubingwa wa mashindano yote na kuwapa Namungo Fc kumaliza nafasi ya pili katika kombe la shirikisho.

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzani amethibitisha hilo mara baada ya mchezo wa juzi kumalizika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala