Connect with us

Makala

Simba Wazitaka Tatu Za JKT

Kikosi cha Simba Sc kimesema kuwa kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo utakaopigwa uwanja wa Jamhuri dhidi ya JKT Tanzania ikiwa ni mchezo wa raundi ya tano ligi kuu bara.

Simba Sc iliyochini ya kocha mkuu Sven Vandernbroeck watakutana na JKT Tanzania majira ya 1:00 usiku ambapo matarajio yao makubwa ni kupata matokeo chanya licha ya muda mrefu kutotumia uwanja huo.

Mchezo huo utakuwa ni wa ushindani mkubwa kwani wote wanazihitaji pointi tatu ikiwa Simba wametoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar huku JKT Tanzania wakiwa wamefungwa bao 1-0 na Coastal Union.

JKT Tanzania ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 4 kibindoni inakutana na Simba iliyo nafasi ya 3 na pointi 10.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala