Connect with us

Makala

Simba Sc,Pamba Jiji Fc Watozwa Faini

Bodi ya ligi kuu nchini imewatoza faini ya Shilingi milioni tano kila mmoja klabu za Simba sc na Pamba Jiji Fc kutokana na kuvunja kanuni siku moja kabla ya mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo Novemba 22 mwaka huu.

Katika mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba jijini Mwanza na Simba sc kuibuka na ushindi wa 1-0 likifungwa kwa penati na Lionel Ateba,siku moja kabla ya mchezo kulitokea sintofahamu wakati Simba sc wakiwa mazoezini ambapo maofisa wa klabu ya Pamba Jiji walivamia mazoezi hayo na kujifungia katika moja ya vyumba vilivyopo ndani ya uwanja huo.

Maofisa wa klabu ya Simba Sc walivunja moja ya vioo vya dirisha la vyumba hivyo wakijaribu kuwatoa maofisa wa Pamba Jiji hali iliyoleta Tafrani na kusababisha Polisi kuingia kudhibiti vurugu hizo.

Katika adhabu hiyo iliyotolewa na Bodi ya ligi kuu pia Simba sc inapaswa kuwasiliana na wamiliki wa uwanja kwa ajili ya kufanya ukarabati wa uharibifu huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala