Connect with us

Makala

Simba sc Yazindua Jezi

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kufanya uzinduzi wa jezi maalumu kwa ajili ya michuano ya kimataifa zenye nembo ya Visit Tanzania ambazo zitaanza kupatikana madukani kuanzia Februari 15 mwaka baada ya mzigo wa jezi hizo kuwasili nchini.

Uzinduzi wa jezi umefanyika katika hoteli ya Serena na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa michezo ikiwemo Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii huku jezi hizo zikipata baraka ya wadhamini wa sasa wa klabu hiyo kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-bet.

Jezi hizo zipo kati seti tatu tofauti za nyumbani,ugenini na zile za kati huku pia bei za jezi hizo kwa rejareja itakua kiasi cha shilingi elfu thelasini na tano tu.

“Tukisafiri tutakuwa na M-Bet, siku moja kabla ya mechi na siku ya mechi ndio tutakuwa tunatumia Visit Tanzania kama ilivyo matakwa ya CAF.”

“Jezi zitauzwa Tsh. 35,000 kwa jezi moja na zitaanza kuuzwa Februari 15, 2023. Wachezaji wataanza kuvaa tukienda kucheza na Horoya.” Alisema Meneja wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Ahmed Ally.

“Tunaishukuru Bodi ya Utalii kwa kuturuhusu kutumia neno Visit Tanzania ili kuitangaza nchi yetu. Historia ya Simba ni kubwa na ndio klabu pekee nchini ambayo inaweza kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi.”

“Lakini pia tunamshukuru mwekezaji wetu Mo dewji kwa kazi kubwa anayoifanya. Pia nichukue nafasi hii kuwapongeza watu wote walioshinda kwenye uchaguzi wa Simba.Alisema muwakilishi wa Mdhamini wa klabu hiyo, Adam Mgoyi.

Simba sc inatarajiwa kusafiri hivi karibuni kuelekea nchini Guinnea kuvaana na Horoya Fc katika mchezo wa kwanza wa kombe la klabu bingwa barani Afrika siku ya Jumamosi Februari 11 na kisha ikirejea itavaana na Raja Casablanca katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala