Connect with us

Makala

Simba Sc Yawashangaza waarabu Dar

Bao la ushindi la dakika ya 90+7″ lililofungwa na Kibu Dennis limezua tafrani baada ya kuipatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Cs Sfaxien ya nchini Tunisia katika mchezo wa makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika uliofanyika Disemba 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba sc ikiruhusu bao la mapema dakika ya 3’ya mchezo likifungwa na Hazem Hassen kutokakana na kosa la kizembe la beki Che Malone Fondoh aliyetaka kumpindua mshambuliaji huyo lakini Kibu Dennis alifanyiwa faulo nje kidogo ya eneo la penati na Jean Charles Ahoua alipiga faulo hiyo kiufundi na mpira kumkuta Kibu aliyekua hajakabwa na kufunga kwa kichwa dakika ya 7′ ya mchezo huo.

Mchezo huo ulianza kuwa na kasi ndogo baada ya kila timu kupata bao ambapo mpaka mapumziko matokeo yalikua hivyo hivyo.

Kipindi cha pili Simba sc ilifanya mabadiliko ya kumuingiza Steven Mukwala na kumtoa Lionel Ateba ili kuongeza kasi huku pia Joshua Mutale akiingia lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda mpaka baadae alivyongia Chamou Karabou na Yusuph Kagoma ambao waliimarisha timu kuanzia nyuma.

Yusuph Kagoma alipiga pasi ndefu iliyounganishwa na Kibu Dennis kwa kichwa dakika ya 90+7’na kuzua shangwe kwa mashabiki wa Simba sc huku mastaa wa Sfaxien wakianzisha vurugu kwa kushambulia mwamuzi wakidai amechelewa kumaliza mpira.

Kutokana na ushindi huo sasa Simba Sc imefikisha alama sita katika msimamo wa Kundi A ambapo wanalingana alama na Fc Bravo na Fc Constantine huku Sfaxien wakishika mkia.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala