Kufuatia kupata Suluhu dhidi ya Klabu ya Simba Sc katika mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mastaa wa klabu ya Al ahly Tripol wamechanganyikiwa kutokana na matokeo hayo.
Licha ya kucheza mbele ya mashabiki wao waliojaa kwa wingi uwanjani hapo lakini hawakuamini macho yao baada ya mwamuzi kumaliza dakika 90 za mchezo huo wa kwanza kwa kila timu kutopata bao huku Simba sc wakiwa na faida ya kuja kumalizia mchezo huo nyumbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 22.
Mashabiki wa Tripol waliamua kurusha chupa kwa hasira huku wakionyesha wazi kutopendezwa na mwamuzi ambaye walidai aliibeba Simba sc kutokana na kukataa kutoa penati baada ya beki wa Simba sc Che Fondoh Malone kuokoa mpira kwa kulala ndani ya eneo la hatari ambapo mashabiki walidhani kuwa ni penati.
Kocha Mkuu wa klabu ya Simba Sc Fadlu Davis alisema tangu awali kuwa anakwenda kuzuia zaidi kwa lengo la kupata sare ama kufungwa idadi ndogo ya mabao ili aje amalizie mchezo huo nyumbani jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Tripoli wamemtaja mwamuzi wa mchezo huo kuwa ndie mchezaji bora wa mchezo huo huku uongozi wa timu hiyo ukipanga kupeleka malalamiko Caf wakidai kuwa hawajatendewa haki.
Kwa upande wa Uongozi wa Simba sc wenyewe umepanga kupeleka malalamiko Caf kutokana na kufanyiwa vurugu na Mashabiki wa klabu hiyo huku mchezaji Aishi Manula akiripotiwa kupigwa na watu wa usalama akiwa jukwaani.
Kla