Connect with us

Makala

Simba Sc Yawaita Mashabiki Adhabu Caf

Klabu ya Simba Sc imeanzisha kampeni maalumu yenye lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi milioni mia moja ambazo zitatumika kulipa faini kwa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) baada ya mashabiki wa klabu hiyo kufanya vurugu katika mchezo dhidi ya Cs Sfaxien uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mchezo huo Simba Sc iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo dakika za mwishoni iliibuka vurugu iliyoanzishwa na mashabiki wa Sc Sfaxien huku wale wa Simba sc wakijibu mashambulizi kwa kuwarushia viti.

Caf baada ya kujiridhisha imeifungia klabu hiyo kucheza na mashabiki kwa mchezo mmoja pamoja na faini ya kiasi cha dola elfu 40 ambazo ni zaidi ya Shilingi milioni mia moja za kitanzania.

Katika kuzindua kampeni hiyo,Meneja wa idara ya habari ya klabu hiyo Ahmed Ally amesema kuwa wameamua kufanya hivyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa baadhi ya mashabiki.

“Tumekuja na kampeni maalumu ambayo hii imeombwa na amshabiki wenyewe wakitaka kuwajibika baada ya kufanya makosa yale. Tumewaletea mfumo wa kuchangia ili kitakachopatikana twende tukalipe faini na Simba Sports Club ibaki salama na kampeni hiyo tumeipa jina la TUNAWAJIBIKA PAMOJA”,Alisema Ahmed akizungumza na waandishi wa habari.

“Natoa rai kwa Wanasimba, asijekutokea mwanasimba wa kuchangisha kwamba kikifika kiasi fulani tutapeleka ofisini. Kila Mwanasimba atume fedha yake moja kwa moja kwenye namba ya ofisi ambayo imetolewa”,Aliendelea kusema kwa msisitizo zaidi.

“Zoezi letu tumeliweka kwa muda sio kwa kiwango kwahiyo kama ikifika milioni 100 na muda bado tutawaachia. Wanasimba wanapaswa kuonyesha nguvu yao, wanapaswa kusimama na timu yao”,Alimalizi Ahmed Ally ambaye sasa amefkisha miaka mitatu ofisini tangu aajiriwe kama mkuu wa Idara hiyo.

Mpaka sasa baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo tayari wameshaanza kutuma michango hiyo kupitia namba tajwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala