Connect with us

Makala

Simba sc Yatua kwa Mmorroco wa Apr

Klabu ya Simba sc ipo katika mazungumzo na kocha Adil Erradi raia wa Morroco kwenda kuchukua nafasi ya kocha Pablo Franco ambaye wamemtimua klabuni hapo hivi leo.

Kocha huyo ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya APR ya nchini Rwanda tayari yupo nchini toka juzi akijadiliana na mabosi wa klabu hiyo kuhusu kusaini mkataba huku akiaga nchini Rwanda kwa mapumziko mafupi.

Simba sc inahitaji kocha mpya baada ya kumtimua Pablo kwa kigezo cha kutofika malengo yaliyopo katika mkataba wake aliousaini wakati akiwa anawasili klabuni hapo akitakiwa kuifikisha timu hiyo nusu fainali ya michuano ya kimataifa na kuchukua makombe mawili ya ligi kuu na kombe la shirikisho la Azam ambapo mpaka sasa kote huko ameshindwa kufanikisha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala