Connect with us

Makala

Simba Sc Yatua Kigoma Kuivaa Mashujaa Fc

Msafara wa kikosi cha timu ya Simba sc umefanikiwa kuwasili salama mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Nbc nch8ini dhidi ya Mashujaa Fc utakaofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo.

Simba sc iliwasili kwa kuchelewa kutokana na uhaba wa viwanja vya kufanyia mazoezi mkoani humo ambapo baada ya kuwasili jana jioni ilifanya mazoezi uwanjani hapo na leo itaingia uwanjani kutafuta alama tatu muhimu dhidi ya klabu hiyo.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na kila timu kuhitaji alama tatu muhimu ili kujikwamua katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini.

Mpaka sasa klabu ya Simba Sc ina alama 19 ikicheza michezo nane ya ligi kuu katika nafasi ya pili ikiachwa alama tano na Yanga sc iliyo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu huu Mashujaa Fc wakiwa nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 13 katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala