Klabu ya Simba sc imeendelea kujiimarisha kuelekea katika msimu wa ligi kuu ujao ambapo imefanikiwa kukamilisha usajili wa majembe mawili ya haraka haraka ili kuboresha maeneo yake ya ulinzi na kiungo.
Simba sc katika usajili huo wikiendi hii iliwatambulisha Aubin Kramo na beki Che Fondoh Malone usajili ambao umeteka hisia za mashabiki wengi wa klabu hiyo ambao bado wanatamba kuwa msimu ujao lazima wabebe makombe yote.
Kramo ambae ni winga amesajili kutoka klabu ya Asec Mimosa ambako alikua amemaliza mkataba wake akiisaidia timu yake msimu uliopita kufika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho nchini michuano ambayo alimaliza akiwa na magoli matano na asisti mbili.
Pia mchezaji huyo anayeweza kucheza winga zote mbili kwa ujumla ameitumikia Mimosa katika michezo 28 akifunga mabao nane na kusaidia upatikanaji wa mabao mawili.
Pia Simba sc imefanikiwa kumsajili mchezaji bora wa ligi kuu ya soka ya Cameroon Che Fondoh Malone ambaye ni beki wa kati akichukua nafasi ya Joash Onyango ambaye ametambulishwa katika klabu ya Singida Fountain Gate Fc.
Malone ambaye tetesi za kusajiliwa Simba sc zilianza muda mrefu huku pia akihusishwa na klabu kadhaa za barani Ulaya lakini nguvu kubwa ya fedha za usajili za Simba sc zilifanikiwa kukamilisha dili hilo na hatimaye kutambulishwa.