Connect with us

Makala

Simba sc Yamkataa Morrison

Mabosi wa klabu ya Simba sc wamekubaliana kuachana na staa Benard Morrison mwishoni mwa msimu huu huku Nidhamu ikiwa ni kigezo kikubwa walichozingatia katika kufikia shauri hilo.

Mabosi hao walifikia maamuzi hayo kutokana na matukio kadhaa ya mshambuliaji huyo licha ya kuwa na nyakati nzuri za kuibeba timu hiyo tangu imsajili kutokea Yanga sc misimu miwili iliyopita.

Inaelezwa kocha Pablo Franco hapendezwi na wingi wa matukio ya nje ya uwanja ya staa huyo hasa kutokana na kuathiri mwenendo wa timu kwa ujumla huku klabu hiyo ikijipanga kusajili wachezaji wa maana ili kuwasaidia katika michuano ya kimataifa.

Hata hivyo tayari inasemekana baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga sc wameanza mazungumzo na staa huyo ili kumrejesha klabuni hapo baada ya kuondoka misimu miwili iliyopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala