Connect with us

Makala

Azam Fc Yatinga Fainali Shirikisho

Azam Fc imefanikiwa kuifunga Simba sc kwa mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho la Azam Sports  uliofanyika katika uwanja wa Nagwanda Sijaoni mjini Mtwara.

Mchezo huo uliokua na kasi ya kusisimua ulihudhuriwa na mashabiki wengi hasa kutoka mikoa hiyo ya kusini huku Simba sc ikianzisha kikosi kile kile kilichoipa ushindi dhidi ya Yanga sc kikiwa na mastaa kama Jean Baleke,Cletous Chama,Saido Ntibanzokiza na Kibu Dennis huku eneo la kiungp likiwa chini ya Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin na Kipa Ally Salim akisimama langoni akisaidiwa na mabeki Shomari Kapombe,Mohamed Hussein,Joash Onyango na Henock Inonga.

Azam Fc yenye ilianza na Kipa Idriss Abdulai,Lusajo Mwaikenda,Bruce Kangwa,Daniel Amoah na Abdalah Mfuko huku eneo la katikati likiwa na Issa Ndala,Ayoub Lyanga na Sospeter Bajana huku James Akaminko,Idriss Mbombo na Abdul Sopu wakiongoza eneo la ushambuliaji.

Azam Fc walipata bao dakika ya 21 likifungwa na Lusajo Mwaikenda baada ya kipa Ally Salim kushindwa kuudaka mpira wa faulo uliomgonga na kumkuta mfungaji lakini dakika saba baadae Sadio Kanoute alisawazisha bao hilo kwa kichwa dakika ya 28 na mpaka mapumziko mechi ilikua sare ya 1-1.

Kipindi cha pili kila timu ilijitahidi kushambulia kitafuta bao la pili lakini uimara wa safu za ulinzi ulikua thabiti huku kuingia kwa Prince Dube kuliwatikisa Simba sc ambao walisababisha mshambuliaji huyo kuifungia timu yake bao la pili baada ya Joash Onyango kushindwa kumkaba akimuacha akiambaa na mpira pembeni ya uwanja na kumtungua kipa Ally Salim dakika ya 78.

Mpaka dakika tisini zikimalizwa na mwamuzi Tatu Malogo Azam Fc iliibuka na ushindi na kufuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo huku Simba sc sasa ikiwa na asilimia kubwa za kumaliza msimu bila taji lolote.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala