Connect with us

Makala

Simba sc Yakusanya 60m Ujenzi wa Uwanja

Meneja mawasiliano wa klabu ya Simba sc Ahmed Ally amesema kwamba klabu hiyo imekusanya jumla ya kiasi cha Tsh 60 milioni pekee kwa ajili ya ujenzi wa uwanja ikiwa ni michango ya mashabiki na wadau mbalimbali tangu mwezi desemba mwaka jana.

Ahmed aliyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘nani zaidi’ kati ya klabu hizo mbili ikiwa na lengo la kuwashindanisha mashabiki kuchangia klabu hizo kupitia nia ya mtandao ya  Azampay.

“Michango hii iko salama na tunawashukuru wanachama na mashabiki ambao wameendelea kuchanga,hakuna pesa ambayo itakwenda kutumika kwenye malengo tofauti,amesema Ahmedi.

“Hatuwezi kusema hizi Sh60 milioni tunaweza kujenga uwanja, safari bado ndefu lakini sasa bado tunataka nguvu zaidi ya michango ya Wanasimba,”Alisema Ahmed

Aidha klabu hiyo imesema kwamba michango hiyo watakayokusanya kupitia uchangiaji huo kwa njia ya mtandao watazipeleka pesa hizo katika ukarabati wa miundombinu ya klabu ikiwemo ujenzi wa uwanja.

“Hela zote ambazo tutapata tutapeleka kwenye ujenzi wa uwanja. Mimi nilienda Doha, Qatar na Mwenyekiti wetu alienda Uturuki kuangalia viwanja.”

“Baada ya Msimu huu Simba itangaza kile ambacho wanakwenda kukijenga. Ni aibu Simba na Yanga hadi Sasa kutokuwa na miundombinu ya viwanja vyao” Barbara Gonzalez CEO Simba SC.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala