Connect with us

Makala

Simba sc Yaifuata Yanga sc Shirikisho

Klabu ya Simba sc sasa itakutana na Yanga sc katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho baada ya kufanikiwa kufuzu kufuatia kuifunga Pamba sc kwa mabao 4-0 katika mchezo uliomalizika usiku huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo uliokua wa upande mmoja kufuatia Pamba sc kuzidiwa kila kitu na Simba sc ambapo Peter Banda alifungua karamu ya mabao akifunga la uongozi dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza na kuifanya Simba sc kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao moja na kipindi cha pili Kibu Dennis alifunga dakika ya 48 huku Yussuph Mhilu akifunga mabao mawili dakika za 53 na 88 na kuipa ushindi mnono Simba sc.

Kutokana na ushindi huo sasa ni dhahiri Simba sc na Yanga sc zitakutana katika mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo ya kombe la shirikisho ambapo Yanga sc ilitangulia kufuzu wakiifunga Geita Gold Fc kwa mikwaju ya penati.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala