Connect with us

Makala

Simba sc Yafungwa Guinnea

Klabu ya Simba sc imeshindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika ikikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Horaya katika mchezo uliofanyika nchini Guinnea.

Simba sc ilifungwa bao hilo kwa kichwa dakika ya 18 ya mchezo likifungwa na Pape Ndiaye na lilidumu mpaka dakika tisini za mchezo licha ya jitihada za Simba sc kusawazisha bao hilo kushindikana huku John Bocco akikosa takribani nafasi mbili zawazi na Horoya wakikosa penati iliyookolewa na Kipa wa Simba sc Aishi Manula.

Pamoja na Simba sc kuanza mchezo na viungo watatu wa ukabaji Mzamiru Yassin,Sadio Kanoute na Sawadogo walishindwa kutawala mchezo ambapo walichangamka baada ya kuingia kwa Bocco,Kibe Dennis na Habib Kyombo lakini mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo huo.

Simba sc sasa inawasubiri Raja Casablanca katika mchezo wa pili utakaofanyika wikiendi ijayo katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

 

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala