Connect with us

Makala

Simba Sc Yafungiwa Kuingiza Mashabiki

Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) limeifungia klabu ya Simba kucheza mechi moja ya CAF bila mashabiki na kulipa kiasi cha dola 40,000 sawa na Tsh milioni 101 kutokana na vurugu zilizojitokeza katika mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien uliopigwa Disemba 15, 2024 simba ikiondoka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam mashabiki wa Simba sc na wale wa Sc Sfaxien walipigana na kuvunja viti baada ya Simba Sc kupata bao la pili kwa kichwa cha Kibu Dennis dakika ya mwisho ya mchezo huo.

Caf baada ya kujiridhisha moja kwa moja imechukua hatua hizo ili kudhibiti nidhamu viwanjani huku ikipunguza adhabu hiyo kutoka mechi mbili mpaka moja kutokana na kuwa kosa la kwanza kwa klabu hiyo.

Kwa maamuzi hayo klabu ya Simba imesitisha mauzo ya tiketi ya mchezo dhidi ya CS Constantine na mashabiki ambao wameshanunua tiketi, tiketi hizo zitatumika kwenye mchezo ujao wa robo fainali.

Simba sc ikiwa tayari imeshafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo itahitaji kushinda mchezo huo ili kuongoza kundi hilo ili kupata faida ya kutopangwa na timu kubwa zenye nguvu ya usajili katika ligi hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala