Connect with us

Makala

Simba sc Yabeba Alama 3 Mbeya

Tofauti na msimu uliopita Simba sc imefanikiwa kupata alama tatu katika mchezo wake wa kwanza nje ya mkoa wa Dar es salaam baada ya kuifunga Prisons Fc 1-0 bao la dakika ya mwishoni lililofunga na Jonas Mkude baada ya mpira wa faulo wa Shomari Kapombe kurudishwa ndani ukielekea kutoka nje.

Simba sc ilikoswakoswa na Prisons Fc katika sehemu kubwa ya mchezo ambapo kukosekana kwa utulivu katika eneo la ushambuliaji la Prisons Fc ndio lililosababisha Simba sc kupata alama hizo tatu muhimu.

Simba sc katika mchezo huo ilifanya mabadiliko katika eneo la ulinzi kwa kuwaanzisha Shomari Kapombe badala ya Israel Mwenda na Kennedy Juma badala ya Mohamed Outtara huku pia Jonas Mkude akianza badala ya Sadio Kanoute na Habib Kyombo akianza eneo la ushambuliaji na mpaka dakika tisini zinakamilika matokeo yalikua suluhu huku bao likipatikana katika dakika za nyongeza za mchezo.

Kutokana ushindi huo Simba sc sasa itakua imefikisha alama 10 sawa na Yanga sc katika nafasi mbili za juu za msimamo wa ligi kuu nchini wakipishana mabao ya kufunga na kufungwa huku wote wawili watakua na kibarua katika michuano ya kimataifa wikiendi ijayo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala