Connect with us

Makala

Simba sc Yaambulia sare AFL

Klabu ya Simba sc imeambulia sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa kombe la African Football league dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na watu wengi wa mashuhuri akiwemo Rais wa Fifa Gian Infantino na Patrice Motsepe Rais wa Caf.

Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi alishuhudia mchezo huo ambapo dakika 20 za kwanza ulikua wa upande mmoja baada ya Simba sc kutokua imara hasa eneo la kiungo cha ukabaji ambapo Al Ahly itabidi wajilaumu wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi za wazi wakiongozwa na Percy Tau.

Baada ya dakika hizo 20 Simba sc walibadilika na kupanga mashambulizi kwa umakini lakini mpaka karibia na mapumziko ambapo Reda Slim aliipatia Al Ahly bao kutokana na makosa ya walinzi wa Simba sc.

Dakika ya 53 Kibu Dennis alisawazisha kwa kichwa akiunganisha pasi ya Cletous Chama na kuwafanya Simba sc kurudi mchezoni ambapo dakika ya 59 supersub Sadio Kanoute aliongeza bao la pili kwa Simba sc japo bao hilo halikudumu baada ya Kahraba kusawazisha dakika ya 63 ya mchezo baada ya mabeki wa Simba sc kuzembea kuokoa mpira wa faulo.

Simba sc walionyesha uimara zaidi dakika za mwishoni mwa mchezo lakini mipango na maarifa ya Al Ahly ya kutaka kuimalizia mechi nchini Misri iliwakwamisha mara kwa mara.

Sasa timu hizo zitarudiana Jumanne ama Jumatano ya wiki ijayo nchini Misri ili kufahamu timu ambayo itafuzu kwenda hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala