Connect with us

Makala

Simba sc Warejea Dsm,Kocha Aomba Radhi

Kikosi cha wachezaji wa klabu ya Simba sc kimerejea jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Kagera ambapo kilivaana na klabu ya Kagera Sugar katika mchezo  wa kiporo wa ligi kuu ya Nbc ambao Simba sc ilipoteza kwa 1-0 bao likifungwa na Hamis Kiiza dakika ya 71 ya mchezo.

Kikosi hicho baada ya kutua katika uwanja wa ndege jijini Dar es salaam Kocha wa klabu hiyo Pablo Franco aliomba radhi kwa mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kufuatia kupoteza mchezo huo muhimu “Ni matokeo ya kusikitisha na yameniumiza sana,Tulijipanga na kujiandaa vizuri kushinda mechi ile”Alisema mkufunzi huyo wa zamani wa Real Madrid ya nchini Hispania

“Ni wakati mbaya sana kupoteza alama (3) tulizopanga kuzipata,, Niwaombe radhi mashabiki na wapenzi wa timu hii waliokuwa na matumaini ya ushindi wa timu yao dhidi ya Kagera sugar,Tunajipanga kufanya vema michezo ijayo ya ligi na Shirikisho (CAF)”Alisema Pablo.

Simba sc sasa imepoteza michezo miwili kati ya michezo mitatu ya ligi kuu iliyocheza hivi karibuni huku pia ikitoa droo dhidi ya Mtibwa Sugar lakini imesalia nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama 25 huku Yanga sc wakiwa kileleni na alama 35.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala