Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Horoya Ac katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki na viongozi wa serikali.
Simba sc ilikua inahitaji alama katika mchezo huo ili kufuzu baada ya kutofanya vizuri katika michezo miwili ya mwanzo ambapo ilifungwa na Horoya Ac na Raja Casablanca na hivyo kuzua mashaka kama itafuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.
Ikianza na viungo washambuliaji wawili na wakabaji wawili ambapo Cletous Chama akisaidiana na Saido Ntibanzokiza waliwakamata wageni katika eneo la katikati mwa uwanja huku Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute wakiwakamata vilivyo mastaa wa Horoya Ac wakiongozwa na Daouda Camara na Mohamed Wankoye.
Chama alifunga mabao matatu dakika za 10,36 na 70(p) huku Jean Baleke akifunga mabao mawili dakika za 32 na 65 na Sadio Kanoute dakika za 54 na 87 na kuunogesha usiku huo kwa wanasimba baada ya kupata uhakika wa kufuzu robo fainali.
Simba sc sasa imesogea mpaka nafasi ya pili ya kundi C ambapo imefikisha alama 9 nyuma ya Raja Casablanca yenye alama 13 huku Horoya Ac ikiwa na alama 4 na Vipers Fc ikiwa na alama 2 ikishika mkia na zikiwa zimebaki mechi moja kwa kila timu.