Connect with us

Makala

Simba sc Waililia Caf

Uongozi wa klabu ya Simba umepanga kuliandikia barua shirikisho la soka barani Africa CAF kuomba waongezewe idadi ya mashabiki kutoka ile ya awali walioruhusiwa ambayo ni mashabiki 35,000.

Simba sc imekua na bahati kwa shirikisho la soka barani Afrika (Caf) kuwaruhusu kuingiza idadi kubwa ya mashabiki katika michezo yao ya kombe la shirikisho inayofanyika hapa nchini licha ya changamoto ya ugonjwa wa uviko 19.

Klabu hiyo baada ya kuruhusiwa kuingiza mashabiki elfu 35 katika michezo ya awali sasa inaomba nyongeza ya mashabiki elfu 10 zaidi katika mchezo wa mwisho wa kundi D dhidi ya Us Gendamarie ambao Simba sc inatakiwa ishinde ili kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo ni pili kwa ukubwa kwa michuano ya ngazi ya vilabu barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala