Connect with us

Makala

Simba Sc Vs Singida saa 2

Kufuatia kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani sasa mchezo wa ligi kuu baina ya klabu ya Simba sc dhidi ya Singida Fountain Gate Fc utachezwa saa mbili na nusu usiku badala ya saa kumi na mbili jioni ili kupisha muda wa Swala na kufuturu kwa mashabiki na wapenzi wa soka nchini.

Mchezo huo utafanyika katika uwanja wa chamazi jijini Dar es salaam ambapo klabu ya Simba sc imehamia kutumia uwanja huo baada ya uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kufungwa kutokana na kungiwa na shirikisho la soka nchini TFF licha ya fanyiwa ukarabati mkubwa katika eneo la kuchezea.

“Mchezo wetu wa kesho dhidi ya Singida Fountain Gate utachezwa saa 2:15 Usiku ili kutoa muda watu kufuturu Yaani tunawasubiri Singida washibe futari ndo tukawakamue uje wa mtama waliokunywa” Ilisomeka taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa instagram wa msemaji wa Simba sc Ahmed Ally.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala