Connect with us

Makala

Simba sc Kuwavaa Wamalawi

Klabu ya Simba sc imepangwa kuanza na Nyasa Big Bullets ya nchini Malawi katika mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika katika droo iliyopigwa nchini Misri.

Endapo Simba sc itafanikiwa kuitoa timu hiyo basi itakutana na mshindi kati ya Red Arrows ya nchini Zambia na Premiro Agosto ya nchini Angola.

Simba sc ina nafasi kubwa ya kuifunga Nyasa Big Bullets ambayo ipo juu ya kilele cha ligi kuu nchini humo ambayo inaendelea nchini Malawi huku pia ikiwa ni moja ya timu kongwe nchini humo ikianzishwa mwaka 1967 ambapo pia iliwahi kumilikiwa na rais wa zamani wa malawi Bakil Mluzi na kipindi hicho iliitwa Bakili Big Bullets.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala